Niko Dodoma. Nimekaa kwenye ofisi yenye AC kali, kapeti zito, na samani za mbao ngumu.
Mkurugenzi wa Shirika la Umma (Public Institution) ananiangalia kwa tabasamu la ushindi. Wametoka kuzindua jengo jipya la ghorofa 15.
Anajiegemeza kwenye kiti chake na kusema sentensi ambayo nimeisikia mara mia moja, na kila nikiisikia, kengele za hatari (Red Flags) zinalia kichwani mwangu:
“Kaka, tumejitahidi sana. Tumejaza hili jengo kwa 90% na tumeuza nyumba zote za mradi wetu kule Bunju… na hatukutumia Dalali wala Kampuni ya Real Estate hata moja. Tumeokoa hela ya Commission!”
Anategemea nimpigie makofi. Anategemea nimwambie, “Hongera sana Mkurugenzi.”
Lakini namwangalia kwa jicho la kiuchumi, na kumuuliza swali moja ambalo linafuta tabasamu lake:
“Mkurugenzi, huo ‘Ushindi’ unaupima kwa vigezo gani? Kujaza faili za wapangaji leo (Occupancy), au kutengeneza Mto wa Pesa endelevu (Sustainable Cashflow) kwa miaka 10 ijayo?”
Kimya.
Hapa ndipo tatizo la Wawekezaji wengi yakiwamo Mashirika mengi ya Umma Tanzania lilipo. Wanasherehekea “Full Occupancy” (Kujaa kwa jengo) kama ndiyo mstari wa kumaliza (Finish Line).
Ukweli mchungu? Kwenye Real Estate Investment, kupata mpangaji ni Mstari wa Kuanzia (Starting Line).
Leo, nataka tuvunje huu mfupa. Nataka nikuonyeshe kwanini “Kiburi cha Kutotumia Wataalamu” (The Hidden Pride) kinagharimu serikali na wanahisa mabilioni ya shilingi kupitia madeni sugu, wapangaji pasua kichwa, na majengo yanayokufa kifo cha mende.
Twende darasani.
The “Excel Sheet” Trap: Kujaza Jengo vs. Kujaza Benki
Mashirika mengi yanapima mafanikio kwa kuangalia Excel Sheet.
- Unit 1: Imechukuliwa.
- Unit 2: Imechukuliwa.
- Unit 100: Imechukuliwa. Total: 100% Sold/Rented.
Wanaripoti kwa Bodi: “Mission Accomplished.”
Lakini Soko (The Market) linauliza maswali magumu ambayo Excel Sheet haionyeshi:
- Are they the right tenants? (Je, hawa wapangaji wana uwezo wa kulipa, au wameingia kwa sababu kodi ni ndogo?)
- Is the mix strategic? (Je, umeweka Ofisi ya Sheria ghorofa moja na Gym yenye kelele?)
- Sustainability: Je, hawa wapangaji wataweza kulipa kodi ya mwezi wa 6, au wataanza hadithi za “Tunaomba mtuvumilie, cheki haijatoka wizarani”?
Data Halisi (The Scary Numbers): Katika utafiti wangu wa majengo makubwa ya mashirika Posta na Kariakoo:
- Majengo mengi yana Occupancy ya 80-90% kwenye karatasi.
- Lakini Collection Rate (Kusanyaji wa Kodi) ni chini ya 60%.
- Arrears (Madeni): Unakuta mpangaji anadaiwa miezi 12, lakini bado yumo ndani.
Hii siyo biashara. Hii ni Charity. Kujaza jengo na wapangaji wasiolipa ni sawa na kufungua duka na kugawa bidhaa bure. Unajihisi uko “busy”, lakini unafilisika.
The Illusion of “Saving Commission” (Gharama ya Urahisi)
Mkurugenzi anasema: “Hatukutumia Mawakala, tumeokoa 5% ya Commission.”
Sawa. Umelinda 5% ya Marketing Budget. Lakini kwa sababu hukutumia mtaalamu kuchuja wapangaji (Tenant Screening), umepata wapangaji ambao wana Default Rate ya 30%.
Hebu piga hesabu:
- Umeokoa TZS 50 Milioni za Commission.
- Umepoteza TZS 500 Milioni kwa kodi ambazo hazilipiki na gharama za kuwafukuza wapangaji mahakamani (Eviction Costs).
Economic Verdict: Cheap is Expensive. Wakala au Mshauri wa Real Estate (Consultant) halipwi kwa ajili ya “Kufungua mlango na kuonyesha nyumba”. Hiyo ni kazi ya Mlinzi.
Mshauri Analipwa kwa ajili ya Vitu Vikuu 6 ambavyo Timu za Ndani (Internal Teams) mara nyingi zinashindwa kuvifanya kwa ufanisi:
A. Market Positioning (Siyo kila mtu ni mteja wetu)
Timu ya ndani inataka “Jengo Lijae”. Mshauri anataka “Jengo Lipande Thamani”. Mshauri anajua: “Hili jengo ni Premium. Tusiweke biashara za rejareja zinazoleta kelele. Tuweke Corporate HQs pekee.” Hii inalinda hadhi ya jengo (Brand Perception) na inaruhusu kupandisha kodi miaka ijayo.
B. Lead Generation vs. Conversion
Kupokea simu za kuulizia (Inquiries) ni rahisi. Kumfanya mtu atoe Bilioni 1 na kusaini mkataba wa miaka 5 (Closing) ni sanaa na sayansi. Inahitaji Follow-up, Negotiation, na Trust. Timu za serikali mara nyingi zinafanya kazi “Saa 2 hadi Saa 9”. Deals zinafungwa “Saa 12 jioni kwenye kikombe cha kahawa“.
C. Tenant Risk Control (The Gatekeeper)
Hapa ndipo pesa inapookolewa. Mshauri wa nje hana undugu na mpangaji. Anafanya Due Diligence ya kijeshi.
- “Lete Bank Statement ya miezi 6.”
- “Lete barua ya landlord wako wa zamani.”
- “Lete Audited Accounts za kampuni.”
Timu za ndani mara nyingi zinaingiliwa na “Vibali Maalum” au “Maelekezo kutoka Juu”. Mshauri wa nje ni kigingi (Buffer) kinachosema: “Huyu hafai, data zinamkataa.”
D. Lease Structuring (Mkataba Siyo Karatasi Tu)
Mkataba wa pango siyo Template ya kupakua mtandaoni. Mshauri anaweka vipengele vya kulinda mapato:
- Escalation Clauses (Kodi ipande kwa % gani?).
- Service Charge Audits.
- Break Clauses. Hivi vitu ndivyo vinavyofanya jengo liwe na faida (Profitability).
“Lakini Tuna Timu ya Masoko ya Ndani…” (The Internal Blindspot)
Hili ni jibu ninalopewa mara nyingi. “Tuna Idara ya Miliki (Estates Department), kwanini tulipe mshauri?”
Jibu langu: Hata Serikali ya Marekani inatumia Consultants. Siyo kwa sababu hawana wafanyakazi. Ni kwa sababu wanahitaji vitu vinne ambavyo ni vigumu kuvipata ndani ya mfumo wa ajira wa kudumu:
- Speed (Kasi): Mshauri analipwa kwa matokeo (Commission). Asipouza, hali. Hivyo anakimbiza dili usiku na mchana. Mfanyakazi wa ndani mshahara unaingia tarehe 30, iwe jengo limejaa au la. Incentive Structure ni tofauti.
- Specialization (Ubobevu): Mshauri anajua soko la Retail, Office, au Industrial kwa undani. Timu ya ndani inasimamia kila kitu, hivyo inakuwa “Jack of all trades, master of none“.
- Objectivity (Ukweli Mtupu): Mshauri anaweza kumwambia Mkurugenzi: “Bei unayotaka ni kubwa mno, soko halikubali.” Mfanyakazi wa chini anaogopa kumwambia bosi ukweli.
- Accountability (Uwajibikaji): Mshauri ana mkataba wa utendaji (Performance Contract). Akiboronga, unamfukuza na kuleta mwingine.
Maswali Halisi Ambayo Bodi Zinapaswa Kuuliza
Kabla hamjafungua shampeni kusherehekea “We didn’t use agents“, jiulizeni maswali haya ya kiuchumi:
A. What is our WALE? (Weighted Average Lease Expiry)
Hii ni namba inayotisha wengi. Inapima: Wastani wa muda uliobaki kwenye mikataba yote. Kama jengo limejaa, lakini mikataba yote ni ya mwaka mmoja mmoja, jengo hilo lina Risk kubwa. Mwaka ukiisha, unaweza kujikuta na jengo tupu (Mass Exodus). Mshauri mzuri anapambania mikataba mirefu (miaka 3-5) ili kuleta utulivu wa mapato.
B. What is the Churn Rate? (Kiwango cha Kuhama)
Je, wapangaji wanaingia na kutoka kama daladala? Kama kila baada ya miezi 6 mna wapangaji wapya, ina maana kuna tatizo la kimkakati. Gharama za kutafuta wapangaji wapya (Acquisition Costs) zinakula faida yote.
C. Brand Perception: Jengo linaonekanaje sokoni?
Je, jengo lenu linajulikana kama “Jengo la Serikali lenye urasimu” au “Business Hub ya Kisasa”? Wapangaji wa hadhi ya juu (Multinationals, Banks, Telcos) hawaendi kwenye majengo ambayo “brand” yake imechafuka kwa sababu ya Tenant Mix mbovu (mfano: Ofisi za kisasa zimechanganywa na frames za kuuza mitumba).
Brokers vs. Professionals (Tusiweke Wote Kapu Moja)
Naelewa hofu yenu. Kuna “Dalali wa Mtaani” asiye na ofisi, asiye na elimu, na tapeli. Huyu hatufai kwenye miradi ya Bilioni 50.
Lakini msiwachanganye hawa na Professional Real Estate Advisors / Agencies. Makampuni yaliyosajiliwa, yenye data, mifumo, bima (Professional Indemnity), na maadili.
Suluhisho kwa Mashirika ya Umma siyo kujifungia na kufanya wenyewe. Suluhisho ni Smart Outsourcing:
- Competitive Selection: Shindanisheni Mawakala. Chagueni mwenye Track Record ya kujaza majengo kama lenu.
- Defined Deliverables: Mpeni KPI. “Tunataka Occupancy ya 80% ndani ya miezi 6, na wapangaji wawe wa Class A pekee.“
- Technical Scope: Watumieni kwa ushauri wa kitaalamu, siyo tu kutafuta watu. Watumieni kubuni Pricing Strategy na Marketing Mix.
Hitimisho: Kiburi ni Gharama (Pride is Expensive)
Ndugu viongozi wa taasisi, Kujenga jengo ni kazi ya Injinia. Kujaza jengo na kuingiza pesa ni kazi ya Mfanyabiashara (Real Estate Expert).
Msichanganye fani hizi. Kusema “Tumeuza wenyewe bila Agents” inasikika vizuri kwenye hotuba za kisiasa. Lakini kwenye vitabu vya hesabu (Balance Sheet), mara nyingi inasomeka kama fursa iliyopotea, madeni yasiyolipika, na majengo yanayochakaa mapema.
Ushauri wangu: Acheni kiburi cha “Sisi tunajua kila kitu“. Tumieni wataalamu. Lipeni TZS 50 Milioni ya Commission, ili mlinde TZS 50 Bilioni ya Uwekezaji.
Hiyo ndiyo Hesabu ya Kiuchumi (The Real Math).
Swali kwako: Je, umewahi kuingia kwenye jengo jipya la serikali ukakuta limejaa wapangaji, lakini lifti mbovu, wapangaji wanalalamika, na biashara zinafungwa kila siku? Unadhani tatizo lilikuwa nini?
Let’s talk Real Estate Strategy.