Wiki iliyopita nilikaa na mteja wangu mmoja, “Mzee K,” kule Serena Hotel. Mzee K ni mstaafu wa shirika la umma, na ana “Lumpsum” yake nzuri mkononi.
Akaniambia kwa kujiamini: “Kijana wangu, nataka kununua jengo la ghorofa 3 Sinza, nifanye commercial, nipangishe fremu na ofisi. Real Estate hailali, si ndio?”
Nilimwangalia. Nikanywa maji. Nikamuuliza: “Mzee, unataka kununua jengo hilo ili uweke heshima mtaani, au unataka kununua ‘Cashflow Engine’?”
Alishindwa kujibu.
Na hapa ndipo 90% ya wawekezaji wa Kitanzania wanapopoteza mabilioni. Tunaamini msemo wa kizamani: “Ardhi haiozi.” Ni kweli haiozi, lakini inaweza kukufilisi.
Cyrus McCormick, tajiri wa Chicago, alitajirika kwa kununua mji kabla haujajengwa. Lakini Dar es Salaam ya 2025 sio Chicago ya 1800. Dar es Salaam ni soko lenye Volatility (Uyumbe), Regulatory Friction (Kodi na Sheria), na Supply Glut (Uwingi wa majengo) katika maeneo fulani.
Kabla hujasaini hundi ya hiyo “Commercial Property,” lazima ufanye Forensic Due Diligence. Usinipe majibu ya haraka.
Kaa chini, piga hesabu. Haya hapa ni maswali 6 ya kikatili unayopaswa kujiuliza kabla hujaingia kwenye soko la Commercial Real Estate la Bongo.
Buckle up. We are going deep.
Swali #1: Cash Flow vs. Appreciation (Je, Unataka Ule Leo au Ule Kesho?)
Hili ndilo kosa la kwanza la kiuchumi (“Original Sin”) la wawekezaji wengi. Hujui unatafuta nini.
Kwenye Real Estate, faida inakuja kwa njia mbili:
- Cash Flow (Kodi): Pesa inayoingia kila mwezi/mwaka kuweka mezani.
- Appreciation (Kupanda Thamani): Pesa unayopata siku ukiuza jengo miaka 10 baadaye.
The Dar es Salaam Reality: Hapa Bongo, mara nyingi hizi mbili haziendi pamoja. Ni “Trade-off.”
Scenario A: The “Mbweni/Kigamboni” Play (Appreciation)
Unanunua eka 5 Kigamboni maeneo ya Cheka au Kimbiji. Bei ni nafuu leo. Lakini Cash Flow ni Sifuri. Hakuna mtu atapanga ofisi kule leo. Unaweka pesa, na unasubiri (Praying) daraja likamilike, mji ukue, ili uuze kwa faida miaka 7 ijayo. Hii inahitaji uwe na “Deep Pockets” (Mifuko mirefu) ya kuishi bila kutegemea hiyo mali.
Scenario B: The “Sinza/Kariakoo” Play (Cash Flow)
Unanunua jengo Sinza au Kariakoo. Bei ni Ghali mno (Premium Entry Price). Lakini Cash Flow ni Kubwa. Fremu moja ya Kariakoo inalipa TZS 3M – 5M kwa mwezi. Hapa unapata pesa ya kula leo. Lakini, thamani ya jengo hilo haitapanda kwa kasi kubwa sana (Cap Rate Compression) kwa sababu tayari imeshafika kileleni (Peaked).
The Trap: Mwekezaji anachukua mkopo wa Benki (Riba 18%) kununua kiwanja Mbweni (Appreciation asset) akitegemea kilipe mkopo.
Matokeo: Nyumba haipati mpangaji, Benki inapiga mnada. Lazima uamue: Unataka Kodi ya Leo (nenda kwenye High Density Areas na ulipe ghali) au Utajiri wa Kesho (nenda Satellites na ukae na njaa)? Usichanganye madesa.
Swali #2: Liquidity Check (Je, Pesa Yako Inaweza Kutoka Jela?)
Real Estate ni Illiquid Asset. (Mali isiyogeuzika pesa haraka). Hii inamaanisha nini kwa lugha ya mtaani? Nyumba ni Jela ya Pesa.
Ukiweka Milioni 500 kwenye jengo la ofisi Mikocheni, hiyo pesa imefungwa. Ikitokea dharura (Emergency)—ugonjwa, kesi, au fursa nyingine ya biashara—huwezi kwenda kwenye ukuta wa jengo na kusema “Naomba Milioni 50 kwenye tofali hizi.”
Uhalisia wa Dar es Salaam: Kuuza “Commercial Property” Dar es Salaam kunachukua wastani wa Miezi 6 hadi Miaka 2. Nimeona majengo Posta yakiwa na bango la “FOR SALE” kwa miaka 3. Kwanini? Kwa sababu wanunuzi wenye Bilioni 2 taslimu hawapo wengi.
The Pango Strategy: Kama unajua utahitaji hiyo pesa ndani ya miaka 3, USINUNUE. Weka kwenye Government Bonds (UTT/BOT) ambazo ni Liquid. Kama unanunua Real Estate, hakikisha una “Emergency Fund” ya miezi 12 pembeni. Usifanye kosa la kuweka “Liquidity” yako yote kwenye matofali. Cash is King, but Bricks are a Dictator.
Swali #3: Risk Tolerance (Je, Unaweza Kuhimili “Kariakoo Strike”?)
Uwekezaji wa majengo ya biashara unaonekana “Safe.” Lakini una hatari zake (Risks). Je, umepima kifua chako?
Risk 1: The Vacancy Risk (Hatari ya Kukosa Mpangaji)
Angalia majengo mapya ya “Morocco Square” au “Palm Village.” Angalia minara ya Posta Mpya. Kuna “Oversupply” ya Office Spaces. Je, unaweza kumudu kulipa Land Rent, Property Tax, na Service Charge kwa miezi 12 bila mpangaji? Kama jibu ni HAPANA, wewe huna Risk Tolerance ya kutosha kucheza ligi hii.
Risk 2: The Regulatory Risk (Hatari ya Sera)
Wiki chache zilizopita, tuliona mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo. Maduka yalifungwa. Kama wewe ni mwenye jengo, na mpangaji wako hafanyi biashara kwa sababu ya mgomo au kodi za TRA, nani anakulipa? Mpangaji atakuambia: “Mzee hali mbaya, punguza kodi au nahama.” Kwenye Commercial Real Estate, mapato yako yanategemea uchumi wa mpangaji wako. Uchumi ukiyumba, na wewe unayumba.
My Advice: Kama unategemea kodi hiyo kwa 100% ili uishi (School fees, Chakula), usinunue jengo la biashara linalotegemea mpangaji mmoja mkubwa (Single Tenant Risk). Nunua jengo lenye fremu nyingi ndogo ndogo (Multi-tenant). Mmoja akiondoka, wengine wanabeba jahazi.
Swali #4: Market Trends (Mall Zimekufa, Godowns Zinaishi)
Hapa ndipo unahitaji kuwa na jicho la Mchumi, sio jicho la Dalali. Dalali atakuambia: “Jenga Mall, malls zinalipa.” Uongo.
The Data: Angalia Vacancy Rate ya Malls kubwa Dar es Salaam (ukitoa Mlimani City na Aura Mall). Nyingi zinapumulia mashine. Utamaduni wa mtanzania sio wa “Shopping Mall” kama Marekani. Utamaduni wetu ni “Street Retail” (Vibanda vya barabarani/Fremu). Watu wanataka kushuka kwenye Daladala na kununua dukani, hawataki kupanda lifti ghorofa ya 3 kununua shati.
Trend Mpya (Where the Money is): Pesa sasa hivi ipo kwenye Logistics & Warehousing (Godowns).
Kwa nini?
- Reli ya SGR imeshaanza kazi kikamilifu. Mzigo mwingi utatoka Bandarini kwenda mikoani na nchi jirani.
- Kurasini kumejaa.
- Eneo jipya la dhahabu ni Kibaha, Mlandizi, na Bagamoyo.
Kama una Bilioni 1, usijenge Mall Tegeta. Nenda Kibaha, nunua eka 10, jenga Modern Warehouses. Mahitaji ya kuhifadhi mizigo (Storage) yanakua kwa kasi ya 134% (kwa data za kimataifa, na Tanzania inafuata mkondo huo). Hii ndiyo Trend ya 2025-2030. Usishindane na GSM kwenye Malls. Shindana na Logistics.
Swali #5: Which Industry? (Chagua Vita Yako)
Commercial Real Estate ina vipengele vingi:
- Retail (Maduka)
- Office (Ofisi)
- Industrial (Viwanda/Godowns)
- Hospitality (Hoteli)
- Medical (Hospitali)
Kila sekta ina “Yield” yake na “Headache” yake.
The “Sinza” Model (Mixed Use):
Hii ndiyo “Sweet Spot” ya Dar. Jengo ambalo chini kuna Fremu (Retail – Duka la Nguo, Pharmacy), na juu kuna Makazi (Residential) au Ofisi ndogo.
Kwa nini hii inafanya kazi?
Kwa sababu inagawanya hatari (Diversification). Biashara zikifungwa, wapangaji wa kuishi wapo. Wapangaji wa kuishi wakihama, biashara zipo. Hii inaitwa “Recession-Proof Asset.”
The “Medical” Niche:
Kuna fursa kubwa sana kwenye kujenga majengo maalum kwa ajili ya Huduma za Afya (Medical Plazas).
Madaktari bingwa wanatafuta sehemu nzuri za kufungua kliniki zao, lakini hawataki kelele za fremu za Kariakoo. Jengo la ghorofa 4, lenye lifti ya wagonjwa (Stretcher Lift), jenereta la uhakika, na maji safi.
Ukijenga hili maeneo ya karibu na Muhimbili, Kairuki, au Hindu Mandal, utajaza madaktari na utapata mikataba ya miaka 10.
Chagua sekta. Usiwe “Jack of all trades.”
Swali #6: Zoning Regulations (Kibali cha Matumizi)
Hili ni bomu linalosubiri kulipuka kwa wawekezaji wengi. Unanunua nyumba ya zamani Oysterbay au Mikocheni. Unataka kuivunja uweke Baa na Car Wash. Unatoa pesa, unanunua. Kesho yake, Manispaa inakupiga STOP.
“Eneo hili ni la Makazi tu (Residential Only).”
Ili kubadilisha matumizi (Change of Use), ni mchakato mrefu, wa gharama, na wakati mwingine hauwezekani. Nimeona wawekezaji wakikwama na majengo ambayo hawawezi kuyatumia kwa biashara, na hawawezi kupata kodi ya kutosha kama makazi kurudisha mtaji wao.
The “Title Deed” Audit: Kabla hujatoa senti tano, chukua Hati. Nenda Wizara ya Ardhi. Angalia “Use of Land.” Kama imeandikwa “Residential,” na wewe unataka “Commercial,” anza mchakato wa Change of Use KABLA ya kununua (iwe condition ya mkataba).
Pia, angalia “Open Spaces” na “Road Reserves.” Dar es Salaam imejaa matapeli wanaouza viwanja vya wazi vya serikali. Bomoa bomoa ikija, hakuna fidia.
Rule: Don’t fight the City Plan. You will lose.
Hitimisho
The Verdict
Kuwekeza kwenye Commercial Real Estate Dar es Salaam ni mchezo wa “High Stakes.” Ukipatia, unajenga utajiri wa vizazi (kama Bakhresa, Mengi, Dewji). Ukikosea, unazika pesa zako kwenye kaburi la simenti.
Kanuni yangu kama Founder wa Pango ni hii: Data over Emotions.
- Usinunue jengo kwa sababu linaonekana zuri.
- Nunua jengo kwa sababu Namba zinaeleweka (The Numbers Make Sense).
Maswali haya 6 ndiyo “Filter” yako. Yakikujibu “Ndio” yote, weka pesa. Yakikupa “Hapana” au “Sijui,” rudisha pesa mfukoni.
The market is ruthless to the ignorant, but generous to the informed.
Kama kawaida yangu, simalizii bila kukupa…
Homework
Unataka kununua jengo la biashara mwezi huu?
Fanya “Traffic Count”: Kaa mbele ya hilo jengo kwa masaa 4 (Asubuhi na Jioni). Hesabu watu wangapi wanapita? Hesabu magari. Biashara inahitaji miguu ya watu (Foot traffic).
Interview Tenants: Usiongee na mwenye nyumba tu. Ongea na wapangaji wa sasa. Waulize: “Umeme/Maji yakoje? Biashara inaendaje hapa? Mwenye nyumba ni mtu wa aina gani?”
Run the Math: Chukua bei ya jengo. Gawa kwa kodi ya mwaka (Net Income). Kama Yield (Faida) ni chini ya 8-10%, Walk Away. (Bonds zinakupa 12-14% bila stress, kwanini upate 6% na stress za wapangaji?).
Be Smart. Build Wealth.
Nikupe kitu gani kingine…
Karibu Pango.