Ni kawaida kwa mtu ku-bargain anapotaka kununua bidhaa au huduma. Na watanzania tuko vizuri sana kwenye eneo hili.
Lakini vipi inapokuja kwenye suala la nyumba?
Namaanisha unapotaka kupanga nyumba… wengi wenu mnakuwa domo zege. Unamuomba dalali akuombee punguzo wewe ukiwa umejifisha kwenye pembe ya nyumba.
Dalali akakuombee punguzo?
Kwa huruma gani aliyonayo juu yako?
Si ni dalali huyu huyu anayetaka hela ya kiatu na kodi ya mwezi?
Au kwa kuwa mmezunguka wote wiki 2, 3 akila hela zako za kiatu, tayari umemzoea na hiyo unaamini kwamba anakupenda hivyo akakuombee punguzo.
Usijidanganye. Kwake yeye, wewe ni fursa.
Hebu nikuambie ukweli ambao hata madalali hawapendi kuuongelea waziwazi kwenye soko la nyumba hususani Dar es Salaam:
👉 Wapangaji wengi hulipa kodi ya juu kuliko thamani halisi ya nyumba wanayoishi.
Sio kwa sababu wanapenda,
sio kwa sababu wana pesa nyingi,
bali kwa sababu hawajui jinsi ya kuzungumza na mwenye nyumba kwa njia sahihi.
Wengine hujaribu kuomba punguzo…
lakini sauti inakwama kwama,
maneno hayajapangwa vizuri,
hawajihamini kabisa,
na mwisho wa siku wanatoka wakiwa wameambiwa:
“Bei ni hiyo hiyo, kama hutaki kuna wengine wengi.”
Na hapo ndipo safari ya maumivu inaanza.
Kwa Nini Makala Hii Ni Muhimu Sana Kwa Mpangaji wa Leo?
Kwa zaidi ya miaka 20 nimekuwa kwenye sekta ya real estate Dar, nimekaa mezani na:
- Wamiliki wa nyumba wakubwa,
- Wapangaji waliovunjika moyo,
- Dalali wajanja,
- Na familia zilizohama nyumba zaidi ya mara 5 ndani ya miaka 3.
Nimeona kilio cha wapangaji:
- Kodi inapanda ghafla,
- Hakuna nafasi ya kujadiliana,
- Dalali wanakula pesa mara mbili,
- Na wapangaji wanaishi kwa hofu ya “mwaka ukiisha tutapandishiwa”.
Lakini pia nimejifunza kitu muhimu sana:
👉 Bargaining ya kodi sio kipaji wala bahati.
Ni SKILL.
Na skill inafunzwa. Nikiwa na maana kwamba mtu yeyeto anaweza kujifunza ujuzi huu.
Makala hii haijaandikwa kukutia moyo…
Imeandikwa kukupa mfumo (framework) wa kufuata – hatua kwa hatua – ili unapofungua mdomo kuomba punguzo la kodi, usisikike kama muombaji, bali uonekane kama mteja mwenye mantiki.
Na kwa kwa taarifa yako, wenye nyumba wanapenda wapangaji wenye akili nzuri na wanaojiamini. Akigundua ni mtu wa namna hiyo, atakukubalia right away.
Kimoyo moyo, akijiambia “nimepata mpangaji mzuri, nyumba yangu itakuwa salama kuliko Khadija aliyeondoka.”
Na labda niende mbali zaidi nikueleze…
Ukweli Mchungu Ambao Wapangaji Wengi Hawaujui
Wapangaji wengi hudhani mwenye nyumba:
- Hana huruma
- Anatafuta pesa tu
- Hataki kusikia habari za punguzo
Lakini ukweli ni huu:
👉 Wamiliki wengi wa nyumba wana hofu kubwa kuliko wapangaji.
Hofu ya:
- Nyumba kukaa wazi miezi 2–3 bila mpangaji
- Kupata mpangaji jeuri na mwenye makelele mengi
- Uharibifu wa nyumba
- Mlipaji anayesuasua
Kwa hiyo unapojua saikolojia ya mwenye nyumba, bargaining inabadilika kabisa.
Kanuni ya Kwanza ya Bargaining – Usii-ignore
Huwezi kuomba punguzo bila value.
Kama hoja yako ni:
- “Kodi ni kubwa”
- “Maisha ni magumu”
- “Naomba nipunguziwe”
Samahani kusema hivi,
lakini hiyo sio bargaining — huko ni kulalamika.
Na unajua nini… hakuna anayependa mlalamishi. Hata wewe unayesoma makala hii, najua 100% hupendi mtu mlalamishi.
Najua siyo wewe na katu usiwe hivyo.
Na hapa ndipo tunapoingia kwenye moyo wa makala hii ambapo nitakupa MBINU 6 ambazo hazijulikani kwa asilimia 98% ya wapangaji jijini Dar es Salaam.
Najua wenye nyumba watanilaumu kwa kukusanua lakini nalazimika kwa sababu najua maumivu yako.
MBINU#1: Elewa Soko Kabla Hujafungua Mdomo
Hii ndiyo hatua ambayo wapangaji 90% hawajui na hasa wanawake.
Dar es Salaam sio soko moja.
Kariakoo ≠ Mbezi
Sinza ≠ Kigamboni
Kimara ≠ Masaki
Lazima ujiulize:
- Nyumba kama hii katika eneo hili zinaenda bei gani sokoni kwa sasa?
- Je, kuna nyumba nyingi zinapatikana au kuna scarcity?
- Je, kipindi hiki ni high demand au low demand?
💡 Pro Tip (kutokana na experience):
- Januari – Machi: soko linakuwa slow kidogo
- Juni – Septemba: demand inapanda
- Novemba – Desemba: wanachuo wamemaliza shule wanarudi mikoni, hivyo wenye nyumba wanakuwa flexible, (hawataki nyumba zikae wazi mwisho wa mwaka)
Ukizungumza bila data ya soko, unaingia vitani bila silaha.
MBINU #2: Fanya Comparative Research (Usiende Mikono Mitupu)
Kabla ya kuomba punguzo, hakikisha una:
- Angalau nyumba 3–5 za mfano
- Zenye sifa zinazofanana (vyumba, eneo, parking, maji, umeme)
- Bei zake halisi (sio za kusikia)
Sio lazima useme:
“Kwa jirani kodi ni ndogo”
Badala yake sema:
“Nimeangalia nyumba kadhaa eneo hili, nyingi ziko range ya X hadi Y. Ningependa tuone kama tunaweza kukutana katikati.”
👉 Hii ni adult conversation, sio drama.
Najua, unawaza kwa nini yote haya?
Naam, ukweli ni kwamba karibu 20% – 40% ya kipato chako cha mwezi unakitumia kulipia nyumba. Wengi hawajui kuhusu hili kwa sababu wanalipa kodi miezi 6 in advance. Lakini ukweli ndo huo. Jiulize unaingiza mapato au mshahara kiasi gani kwa mwezi na unalipa nyumba kiasi gani. Utajua, hujui 😀
Kumbe, kuomba punguzo ni sehemu ya kuongeza mapato yako ya mwezi.
MBINU #3: Andaa Hoja Zako Kama Business Proposal
Hapa ndipo technique ya ninja inapotumika. Matajiri wanaitumia sana hii…
Usiombe punguzo kama mpangaji maskini.
Omba kama mtu anayejua anachokileta mezani.
Hoja zako ziwe:
- Umekuwa mpangaji mwaminifu
- Hulipi kodi kwa kuchelewa
- Unatunza nyumba vizuri
- Huna usumbufu kwa majirani
- Uko tayari kukaa muda mrefu (long-term tenant)
💡 Truth ya real estate:
Wenye nyumba wanapenda stability, sio kubadilisha wapangaji kila mwaka.
Rafiki yangu mwenye nyumba 9 za kupangisha hapa Dar na Dodoma, akiona wapangaji hawakai muda mrefu… mara moja anaanza kufanya uchunguzi kujua shida ni nini. Kujua tatizo lipo kwake au kwa wapangaji wenyeji?
Na kweli, mara nyingi huwa anagundua kuna mpangaji mmojawapo ni pasua kichwa kwenye nyumba anayewafanya wengine (innocent) waondoke. Anampa notice mara moja na kuomba radhi kwa wengine.
Utarajibu huu, unamsaidia nyumba zake kuwa kimbilio. Muda wote amejaza.
Unayesoma makala hii, kama ni mwenye nyumba… umeshajua SIRI mojawapo ya kufurikisha wapangaji muda wote.
Hakuna uchawi. Nitafute kwa SIRI nyingine.
Tuendelee na…
MBINU #4. Mazungumzo ya Ana kwa Ana (Hii Inabadilisha Kila Kitu)
WhatsApp ni nzuri.
SMS ni rahisi.
Lakini face-to-face ni powerful.
Kwa nini?
Kwa sababu:
- Unasoma body language
- Unajenga trust
- Unapunguza misunderstandings
Anza kwa:
- Kumshukuru
- Kumpongeza kwa nyumba
- Kuonyesha unathamini relationship
Kisha polepole leta hoja.
Usianze na:
“Kodi ni kubwa”
Anza na:
“Nimefurahia sana kuishi hapa, ningependa kuendelea kukaa kwa muda mrefu…”
💡 Pro Tip – Viwashe
Nenda umavalia vizuri (casual but presentable). Kama ni mdada, vaa kama unaenda date fulani hivi na mfanya-bishara mkubwa hapo Kariakoo.
Usivae suti wala nguo fupi. Always, kuwa casual but presentable.
MBINU #5. Tumia Win–Win Language
Hii ni language ambayo watu wachache sana hujua kuitumia.
Badala ya:
“Naomba unipunguzie kodi”
Tumia:
“Ningependa tuone namna ambavyo tunaweza kufanya hii iwe comfortable kwa pande zote mbili.”
Au:
“Kama kuna namna ya kufanya adjustment kidogo, nipo tayari ku-commit kukaa muda mrefu.”
👉 Hapa unauza uhakika, sio huruma.
Kumbuka wewe ni mteja, una hela zako mfukoni. Ongea na namlaka, lakini siyo kwa kumfokea. Mtendeeni sawa sawa na unavyotaka kutendewa.
MBINU #6. Kuwa Tayari Kubargain, Sio Kushinda
Umeenda ku-bargaining sio kupigana vita.
Ni negotiation.
Unaweza:
- Kukubali kulipa miezi mingi upfront
- Kukubali kufanya minor maintenance
- Kukubali increase ndogo badala ya kubwa
Wapangaji wengi (hasa mashabiki wa Simba na Yanga) hupoteza kila kitu kwa sababu wanataka ushindi wa asilimia 100.
Ukweli Mwingine Ambao Hausemwi (Pengine Ndo Mara ya Kwanza Kuusikia)
Wapangaji wengi wanapoteza nguvu ya bargaining kwa sababu:
- Wanategemea dalali
- Hawana direct access kwa mwenye nyumba
- Hawana leverage
Na hapa ndipo Pango App inabadilisha mchezo wote.
Jinsi Pango Inavyokupa Nguvu ya Bargaining (Leverage)
Kwa uzoefu wangu, direct connection ni everything.
Pango:
- Inakuunganisha moja kwa moja na mwenye nyumba
- Inakuondoa kwa madalali wasiokuwa wa lazima
- Inakupa transparency ya soko
Lakini kuna kitu kimoja cha kipekee sana ambacho Pango imefanya, ambacho sijawahi kukiona Dar kabla.
👉 Mpangaji anayetarajia kuhama anaweza kuiweka nyumba kwenye Pango, na akipata mpangaji mpya, anapata 30% ya kodi.
Hii inamaanisha:
- Mwenye nyumba anapunguza gharama
- Mpangaji anapata kipato
- Mpangaji mpya anaingia bila drama za madalali.
Hii ni ecosystem, sio tu app.
Kwa Nini Hii Inasaidia Bargaining?
Kwa sababu:
- Unakuwa sehemu ya solution, sio tatizo
- Unasaidia mwenye nyumba kupata mpangaji
- Unajijengea goodwill
Na kama unavyojua, goodwill = negotiating power.
Baada ya miaka 20 kwenye sekta hii, naweza kusema kwa uhakika:
👉 Kodi haiamuliwi na mwenye nyumba pekee.
Inaamuliwa na mazungumzo.
Na mazungumzo mazuri:
- Yanahitaji maandalizi
- Yanahitaji saikolojia
- Yanahitaji tools sahihi
Kama mpangaji, acha kuogopa kuzungumza.
Kama mwenye nyumba, acha kuona wapangaji kama maadui.
Na kama unataka namna mpya, bora na ya kisasa:
- Bila drama
- Bila madalali wachoyo
- Bila stress zisizo za lazima
👉 Pango sio option tena.
Ni infrastructure ya soko jipya kwa jiji la Tanzania.
Ni zamu yangu kusikia kutoka kwako kupitia comment sections hapa chini. Mbali na maoni yako mengine, ningependa pia kusikia nini unataka tugusie katika makala ijayo.
Uwanja ni wako.