Wiki iliyopita nilikaa na mteja wangu, “Mama K,” ambaye ana Apartments nne maeneo ya Mbezi Beach na Mikocheni. Mama K ni mjasiriamali shupavu. Lakini alikuwa na hasira. Alifungua simu yake, akanionyesha mapato yake ya Airbnb ya mwezi uliopita.
“Kaka, angalia hawa Airbnb wanavyoniibia. Wamechukua karibu Dola 400 kama ‘Service Fee’ na ‘Commission’. Hii ni pesa nyingi sana! Nimeamua nataka kujitoa, nitengeneze Website yangu, wateja waje kwangu moja kwa moja (Direct Booking) ili nile 100% ya pesa yangu.”
Nilimtazama. Nikahema. Nikajua huyu ni mhanga mwingine wa uongo mkubwa zaidi kwenye soko la Hospitality.
Uongo huo unasema: “Direct Bookings are Free.” (Kupata mteja wa moja kwa moja ni bure).
Huu ni uongo ghali sana. Ni uongo ambao umefilisi wenye nyumba wengi Dar es Salaam kuliko hata kodi ya TRA. Wamiliki wengi wanaona ile 15% ya Airbnb kama “Pesa iliyochomwa moto.”
Uhalisia? Hiyo 15% ni gharama nafuu zaidi ya Marketing unayoweza kulipa duniani.
Kama Founder wa Pango, system designer, na web developer niliyeona “Backend” ya biashara hii, nataka nikupeleke darasani leo.
Tutaenda kufanya Forensic Accounting ya Direct Booking vs. OTA (Online Travel Agencies).
Tutavunja namba za gharama za “Website,” “Payment Gateways” za Bongo, na “Customer Acquisition Cost.”
Ukimaliza kusoma hapa, utatamani ungekuwa unailipa Airbnb 20% badala ya 15%.
Buckle up. We are going deep.
The “Commission” Fallacy (Kosa la Kifikra)
Watu wengi wa Dar es Salaam wana “Dalali Mindset.” Tunaamini kwamba mtu wa kati (Middleman) siku zote ni mnyonyaji. Kwamba akiondoka, faida yetu inaongezeka.
Lakini kwenye ulimwengu wa Kidijitali, Airbnb sio Dalali wa kawaida. Airbnb ni “Performance-Based Marketing Agency.”
Fikiria hivi: Unataka kutangaza biashara yako. Unaenda Clouds FM au Wasafi TV. Unawalipa TZS Milioni 2 ili warushe tangazo lako kwa wiki moja. Je, wanakupa uhakika (Guarantee) kwamba wateja watakuja? HAPANA.
Unalipa pesa, tangazo linaruka. Wateja wakija, sawa. Wasipokuja, “Imekula kwako.” Pesa imeenda.
Sasa angalia Airbnb. Wanakuweka kwenye jukwaa lao lenye watumiaji milioni 150 duniani. Wanakuonyesha kwa wageni wanaotafuta “Dar es Salaam.” Wanahost picha zako. Wanakupa mfumo wa malipo.
Na wanakwambiaje? “Usitulipe chochote. Tulipe TU pale mteja atakapolala kwenye kitanda chako na pesa ikawa imeingia.”
Hii inaitwa Cost Per Acquisition (CPA) au Success Fee. Unalipa matokeo, hulipi jaribio. Kwenye uchumi, hii inaitwa “Efficiency.”
Mama K anataka kuacha kulipa “Matokeo” (15%), ili aende kulipa “Matumaini” (Website, Google Ads, SEO) ambazo hazina uhakika. Huko ni kujirusha kwenye shimo la pesa.
The Hidden Cost of “Direct” (Gharama za Kujitegemea)
Hebu tufanye Audit ya nini kinahitajika ili upate “Direct Booking” hapa Dar es Salaam bila kupitia Airbnb. Wengi wanadhani ni kuwa na namba ya simu na ukurasa wa Instagram. Wrong.
Ili uwe na biashara endelevu ya Direct Booking inayoshindana na Airbnb, unahitaji vitu vifuatavyo, na vyote vina gharama (“Price Tag”):
1. Payment Processing Fees (Ada za Malipo)
Airbnb wanakata pesa kwenye kadi ya mteja na kukutumia wewe. Ukijitegemea, lazima uwe na njia ya kupokea pesa. Mteja wa Marekani hatakutumia M-Pesa. Hawezi. Ana Kadi ya Visa au MasterCard. Lazima uunganishe mfumo kama DPO, Selcom, au Flutterwave kwenye website yako.
Gharama: Hawa jamaa wanakata kati ya 3% hadi 4% ya kila muamala (Transaction Fee). Kwa hiyo, ile “Saving” yako ya 15% imeshapungua na kubaki 11%.
2. The “Trust” Deficit (Gharama ya Kuaminika)
Hili ndilo tatizo kubwa zaidi Afrika. Mtalii anayeitwa “John” yuko London. Anataka kuja Dar. Ameona nyumba yako kwenye Website yako binafsi “https://www.google.com/search?q=MamaK-Apartments.com”. Nyumba ni nzuri. Lakini John anasita. Anajiuliza: “Je, huyu mtu siyo tapeli? Nikituma $500 zangu, nikifika Dar nikakuta hakuna nyumba, nitaenda wapi?”
Airbnb inatatua tatizo hili kwa kuwa na “Escrow Agent.” John anajua Airbnb wameshika pesa, na akifika akakuta nyumba mbovu, Airbnb watamrudishia. Wewe “Mama K” huna hiyo Reputation. Ili umshawishi John akuamini wewe moja kwa moja, lazima ufanye kazi ya ziada ya Marketing na Branding ambayo inagharimu pesa nyingi.
3. Tech Stack & Maintenance
Website sio bango la barabarani ambalo unalibandika na kuliacha. Website inahitaji Hosting, Domain, Booking Engine (kama unataka iwe live na isigongane na bookings nyingine), na Security Certificates (SSL). Gharama ya mtaalam wa IT wa kueleweka Dar es Salaam kutengeneza mfumo unaofanya kazi: TZS 1.5M – 3M. Gharama ya Maintenance kwa mwaka: TZS 500,000.
4. Customer Acquisition Cost (CAC) – The Killer
Hapa ndipo hesabu zinapoharibika kabisa. Airbnb wanakuletea wateja bure (mpaka walipie). Kwenye Website yako, nani anajua ipo? Hakuna. Lazima ulipe Google Ads au Instagram/Facebook Ads.
The Math: Wastani wa Conversion Rate kwenye website za mahoteli ni 2%. Yaani, katika watu 100 wanaotembelea website yako, watu 2 tu ndio watabook. Ili upate watu 100 kwenye website yako kupitia matangazo (Ads), na tuseme unalipa $0.50 (TZS 1,300) kwa kila Click (ambayo ni bei ya chini sana kwa keywords za utalii).
Gharama ya Traffic: 100 x $0.50 = $50.
Booking: 2. Gharama ya kupata Booking moja (CAC): $25.
Kama unauza usiku mmoja kwa $80. Umetumia $25 kumpata mteja. Hiyo ni 31% ya mapato yako. Linganisha na 15% ya Airbnb.
Umeona hesabu? Kutafuta mteja mwenyewe (“Direct”) kunagharimu MARA MBILI ya kile unacholipa Airbnb, na bado unahangaika na IT issues.
Scale Matters (Lini Ufanye Direct Booking?)
Je, inamaanisha “Direct Booking” ni mbaya siku zote? Hapana. Inamaanisha ni mbaya KAMA HUNA SCALE.
Nikiwa advisor, nilifanya uchambuzi wa data kutoka kwa operators wakubwa wenye units 400+.
Tuligundua nini?
Gharama halisi ya Direct Booking (Tech + Labor + Ads + Processing Fees) inacheza kwenye 12% – 14%.
Tofauti kati ya 12% (Direct) na 15% (Airbnb) ni 3% tu.
Je, inafaa kupata stress zote za kusimamia website, malipo, na matapeli kwa ajili ya kuokoa 3%? Kwa wengi, jibu ni HAPANA.
Hii 3% ni “Price of Certainty.” (Gharama ya Uhakika). Unalipa Airbnb ili usiwaze kuhusu Credit Card Fraud. Unalipa Airbnb ili usiwaze kuhusu Server Down. Unalipa Airbnb ili usiwaze kuhusu SEO.
Usiwekeze kwenye “Direct Channel” mpaka Brand yako iwe kubwa kiasi kwamba watu wanaitafuta Google kwa jina. Kama watu wanasearch “Apartments in Dar es Salaam,” baki Airbnb. Kama watu wanasearch “Mama K Luxury Homes,” hapo unaweza kuanza website.
The “Pango” Strategy (Jinsi ya Kucheza Mchezo Huu Dar es Salaam)
Sasa, tufanye nini? Tukubali tu kulipa 15% milele?
Hapana. Kama Mchumi, nakushauri utumie mbinu inaitwa “The Trojan Horse Strategy.”
Tumia Airbnb (na Booking.com) kama Timu yako ya Mauzo (Sales Team). Waache wafanye kazi ngumu ya kumleta mteja mlangoni kwako. Lipa hiyo 15% kwa roho safi kabisa kama “Gharama ya Kumleta Mteja” (Acquisition Fee).
Kisha, fanya yafuatayo:
Harvest the Repeat Guest (Vuna Mteja Anayerudi): Mteja akishafika, akalala, akafurahia huduma… hapo ndipo mchezo unabadilika.
Ushajenga Trust. Ameshaona nyumba. Wakati anaondoka, mpe kadi yako ya biashara au kipeperushi.
Andika: “Next time you come to Dar, book directly with us via WhatsApp and get a 10% discount.“
Hesabu Zake:
-
- Unampa punguzo la 10% (Anajisikia vizuri, anaokoa pesa).
- Wewe unaokoa 5% (badala ya kulipa 15% Airbnb).
- Na muhimu zaidi: Unamiliki Mteja (You own the customer data).
Focus on “Corporate Stays” (Wateja wa Makampuni): Dar es Salaam ina wageni wengi wa kikazi (NGOs, UN, Banks). Hawa hawajali sana punguzo la $5. Wanajali Risiti na Uhakika.
Hapa ndipo unapohitaji mfumo wa Direct Booking (hata kama ni Invoicing ya kawaida). Jenga uhusiano na Admin Officers wa makampuni.
Hawa wanaleta wateja wa muda mrefu (Long stays) ambao Airbnb inaweza kuwa ghali kwao kutokana na Service Fees za upande wa mteja.
Build a Great Product First (Jenga Bidhaa Bora): Hakuna Marketing inayoweza kuokoa bidhaa mbovu. Kabla hujawaza website, waza kuhusu mashuka yako. Waza kuhusu AC zako. Waza kuhusu maji ya moto.
Reviews nzuri kwenye Airbnb ndiyo mtaji wako mkubwa. Superhost Status ina thamani kubwa kuliko Website mbovu.
The Verdict (Hukumu ya Mwisho)
Acha kuwaza kuhusu “Kuokoa Commission.” Anza kuwaza kuhusu “Maximizing Occupancy” (Kujaza Nyumba).
Nyumba iliyo wazi inakula 100% ya mapato. Nyumba iliyojaa kupitia Airbnb inakula 15% tu. Bora upate 85% ya kitu, kuliko 100% ya sifuri.
Kwenye soko la Dar es Salaam, ambalo bado linakua na halina “Trust Infrastructure” imara, OTAs (Airbnb/Booking.com) ni Marafiki zako, sio maadui. Wanakupa ulinzi. Wanakupa soko la dunia. Wanakupa mfumo wa malipo.
Usiwe na haraka ya kujitegemea kabla hujakomaa. Direct Channel ni Anasa (Luxury) inayopatikana kwa wale wenye Scale, sio Mahitaji (Necessity) kwa wanaoanza.
Homework
Kama wewe ni Host wa Airbnb Dar es Salaam:
Fungua Excel Sheet yako.
Angalia booking zako za miezi 3 iliyopita.
Hesabu ni wageni wangapi wamerudi mara ya pili (Repeat Guests).
Kama ni chini ya 10%, tatizo lako sio Airbnb Commission. Tatizo ni Huduma Yako (Product). Wateja hawarudi. Wekeza nguvu zako kuboresha huduma, usafi, na ukarimu.
Kama una Repeat Guests wengi, basi anza kutengeneza “Welcome Pack” yenye namba yako ya WhatsApp na ofa ya punguzo kwa safari ijayo. Hapo ndipo unapoanza kujenga Direct Booking polepole, kwa akili, na bila gharama.
Don’t build a website. Build a Brand.
Karibu Pango.