Kuna ugonjwa mkubwa sana unaowatesa wawekezaji wa Kitanzania. Unaitwa “Emotional Investing.”
Unanunua kiwanja Goba kwa sababu “Mji unakua kule.” Unajenga ghorofa Tegeta kwa sababu “Nataka kuacha urithi.” Unajenga nyumba ya kupangisha Sinza kwa sababu “Ardhi haiozi.”
Hizi zote ni hisia. Sio biashara. Na kwenye ulimwengu wa pesa, Hisia zinagharimu.
Mwekezaji mwenye akili (Sophisticated Investor) haangalii uzuri wa nyumba au sifa za mtaani. Anaangalia kitu kimoja tu: Risk-Adjusted Return. Yaani: “Je, faida ninayopata inafidia hatari ninayochukua?”
Hapa ndipo dhana ya Risk Premium inapoingia. Kama huelewi dhana hii, unafanya kazi ya hisani kwa wapangaji wako. Unawapa nyumba ya bei rahisi huku pesa yako ikiliwa na mfumuko wa bei.
Leo, tunaenda kufanya Forensic Breakdown ya Risk Premium katika soko la Tanzania.
Tutavunja namba za Hati Fungani (Bonds), Mfumuko wa Bei (Inflation), na Soko la Nyumba (Rental Yields).
Ukimaliza kusoma hapa, hutaangalia nyumba yoyote kwa jicho lile lile tena.
Buckle up. We are going deep.
Part 1: The “Risk-Free” Benchmark (Kipimo cha Uvivu)
Kabla hujachimba msingi wa nyumba, lazimaujiulize swali moja gumu: “Je, ninaweza kupata pesa ngapi nikikaa tu na kutofanya chochote?”
Hii inaitwa Risk-Free Rate.
Nchini Tanzania, kipimo bora cha hii ni Hati Fungani za Serikali (Government Bonds). Hivi sasa, Bond ya miaka 20 inatoa wastani wa 15.49% (kwa data za hivi karibuni za BOT) na ya miaka 5 inatoa karibu 9-10%.
Hebu tuseme una TZS 500 Milioni. Ukiweka kwenye Bond ya miaka 20 (Risk Free), unapata TZS 77.45 Milioni kila mwaka. Bila kusimamia fundi. Bila kuzibua choo cha mpangaji. Bila kulipa kodi ya ardhi. Bila stress. Unakaa nyumbani, serikali inakuwekea pesa.
Sasa, mtu anakuja anakuambia: “Nunua jengo la biashara Kariakoo kwa Milioni 500.” Jengo hilo lina wapangaji, lina kodi ya TRA, lina uchakavu, lina hatari ya kuungua moto.
Je, unapaswa kukubali kupata faida ya 10% (50M) kwenye jengo hilo? HAPANA.
Kama unapata 15% ukiwa umelala, kwanini upate 10% ukiwa unahangaika?
Hapo ndipo unapoingizwa mjini.
The Inflation Thief (Mwizi wa Kimya Kimya)
Pesa yako ina adui. Anaitwa Mfumuko wa Bei (Inflation). Tanzania, mfumuko wa bei unacheza kwenye 3% hadi 4%. Hii inamaanisha, kila mwaka, thamani ya Shilingi yako inapungua kwa 4%.
Kama uwekezaji wako unakupa 4% faida, Hujatengeneza faida. Umerudisha thamani tu (Breakeven). Faida halisi (Real Return) inaanza kuhesabiwa BAADA ya kutoa inflation.
Formula ya Pango: Risk-Free Rate (Bond) + Inflation Rate = Minimum Hurdle Rate. (Kima cha chini unachopaswa kukubali kabla hujaongeza hatari ya biashara).
Mfano: Bond (10%) + Inflation (3%) = 13%. Kama uwekezaji wowote unakupa chini ya 13%, ni bora ukanunue Bond ulale.
Calculating The “Risk Premium” (Bei ya Stress Zako)
Sasa tunaingia kwenye Real Estate. Real Estate ina hatari (Risks) ambazo Bond haina:
Liquidity Risk: Huwezi kuuza nyumba kesho ukipata shida. Inachukua miezi 6 kuuza.
Vacancy Risk: Mpangaji anaweza kuhama na nyumba ikakaa wazi miezi 3.
Maintenance Risk: Paa linaweza kuvuja, bomba kupasuka.
Regulatory Risk: Serikali inaweza kubadilisha sheria za kodi au matumizi ya ardhi.
Kwa sababu ya hatari hizi, lazima udai malipo ya ziada. Hii ndiyo Risk Premium. Wataalamu wengi wanaweka Risk Premium ya Real Estate kati ya 3% hadi 6% juu ya Risk-Free Rate.
The Golden Formula: Risk-Free Rate (10% – Bond ya miaka 5) + Inflation Buffer (3%) + Risk Premium (3-5%) = Target Return (16% – 18%).
Kwa hiyo, ukijenga “Apartments” za kupangisha Goba, au jengo la ofisi Mikocheni, lengo lako linapaswa kuwa kupata Return on Investment (ROI) ya 16% au zaidi. Kama hesabu zako zinaonyesha utapata 8%, huo siyo uwekezaji. Hiyo ni Sadaka.
The Reality Check (Soko la Dar Likoje?)
Hebu tufanye Audit ya soko la sasa.
Case Study: Nyumba ya Kupangisha Mbezi Beach
Gharama ya Kununua/Kujenga: TZS 400 Milioni.
Kodi kwa Mwezi: TZS 1.5 Milioni ($600).
Kodi kwa Mwaka: TZS 18 Milioni.
Gharama za Uendeshaji (Maintenance, Vacancy, Taxes): TZS 3 Milioni.
Mapato Halisi (Net Income): TZS 15 Milioni.
ROI Calculation: 15M / 400M = 3.75%.
The Verdict: Umemeka 400M kupata 3.75%. Bond ya Serikali inakupa 13-15%. Unapoteza takriban 10% ya mtaji wako kila mwaka kwa “Opportunity Cost” (Gharama ya fursa iliyopotea). Kwa lugha nyepesi: Unajilipua ili uwe Landlord.
Hii ndiyo sababu nasema: Watu wengi wa Real Estate Dar es Salaam ni matajiri wa mali, lakini maskini wa “Cashflow.”
Jinsi ya Kupata Hiyo 16% (The Strategy)
Sasa unajiuliza, “Kane, inawezekana kupata 16% Dar es Salaam?” Jibu ni NDIO. Lakini sio kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Huwezi kupata 16% kwa kujenga nyumba ya kawaida na kupangisha familia moja.
Hizi hapa mbinu za Pango za kuongeza Yield:
Density (Ongeza Msongamano): Badala ya kujenga nyumba moja kubwa ya 400M, jenga “Studio Apartments” 10 kwenye kiwanja hicho hicho.
Kodi ya Studio moja: TZS 300,000.
Jumla kwa mwezi: 3M.
Kwa mwaka: 36M.
ROI: 36M / 400M = 9%. (Bado tupo chini, lakini tumepanda).
Short-Stay (Airbnb): Badala ya kupangisha kwa mwezi, pangisha kwa siku. Nyumba ya Mbezi Beach inaweza kuingiza $80 kwa siku.
Occupancy Rate (Wastani): 60%.
Mapato: $80 x 18 siku = $1,440 (TZS 3.7M) kwa mwezi.
Kwa mwaka: 44M. ROI: 44M / 400M = 11%. (Tunakaribia).
Buy Distressed Assets (Nunua kwa Punguzo): Siri kubwa ya Real Estate ni “You make money when you buy.” Usinunue nyumba ya 400M kwa 400M.
Tafuta nyumba ya mtu aliyekwama (Distressed Seller), inunue kwa 250M.
Ikarabati kwa 50M.
Jumla 300M.
Ipangishe kwa ile ile 18M.
ROI: 18M / 300M = 6%. (Bado ngumu).
Value Add (Ongeza Thamani): Badilisha matumizi. Nyumba ya kuishiigeuze kuwa Ofisi, au Hostel, au Zahanati. Biashara zinalipa kodi kubwa kuliko makazi.
Hitimisho
The Investor’s Mindset
Uwekezaji sio hisia. Uwekezaji ni hesabu. Kama namba hazikubali, USINUNUE. USIJENGE.
Weka pesa zako kwenye Government Bonds au UTT wakati unasubiri dili sahihi la Real Estate ambalo linakupa Risk Premium unayostahili. Kuwa na pesa taslimu (Liquidity) ni uwekezaji pia. Inakupa uwezo wa kununua pale soko linapoanguka (Market Crash).
Usikubali kuwa “Landlord wa Jina” huku ukifa njaa. Dai faida yako. Dai Risk Premium yako.
Homework
Fanya hivi leo:
Chukua thamani ya sasa ya nyumba yako ya kupangisha (Kama ukiiuza leo).
Chukua kodi halisi unayoingiza kwa mwaka (Toa gharama zote).
Gawanya (Kodi / Thamani).
Kama jibu ni chini ya 8%, uko kwenye “Danger Zone.” Anza kufikiria kuuza hiyo nyumba na kuweka pesa kwenye Bonds, au kubadilisha matumizi yake ili iongeze kodi.
Siku zote…
Don’t fall in love with bricks. Fall in love with cashflow.
Karibu Pango.