Miezi 3 iliyopita niliitwa niende Mikocheni. Eneo la kifahari, upepo wa bahari unavuma, na nimekaa na Mzee mmoja, tumuite “Mzee K”. Ana nyumba ambayo kwa hesabu za haraka (Valuation), thamani yake haipungui TZS 850 Milioni.
Mzee K anataka kuuza. Anahitaji “Liquidity”. Anataka kumalizia miradi yake kijijini na kusomesha wajukuu.
Lakini aliniangalia kwa macho makavu na kutoa sharti ambalo nimelisikia mara elfu moja katika miaka yangu 10 ya kazi hii jijini Dar es Salaam:
“Mwanangu, nataka hii nyumba iuzwe. Lakini sitaki bango. Sitaki picha mtandaoni. Sitaki jirani ajue. Sitaki ndugu zangu wajue.”
Nilimwangalia, nikavuta pumzi, na kumuuliza swali la kibiashara: “Mzee, soko la sasa ni gumu (Tight Liquidity). Tukifanya siri, tutapataje ‘The Best Deal’?”
Jibu lake lilikuwa fupi na la kuumiza: “Wakijua nauza, watasema nimefilisika. Na mbaya zaidi, wakijua nimeuza, simu hazitaacha kuita. Kila mtu atataka fungu lake.”
Hapo ndipo nilipogundua tena tatizo sugu la soko letu la Tanzania. Tunaita “The Silent Sale Paradox“.
Watu wengi hawauzi mali kwa kufuata Market Logic; wanauza kwa kufuata Social Fear.
Leo nataka tukate hii ngebe. Nataka nikuonyeshe kwa namba na data halisi jinsi ambavyo “kuuza nyumba kimya kimya” bila mkakati (Strategy) kunavyokugharimu mamilioni ya shilingi, na jinsi unavyoweza kuuza kwa siri BILA kupoteza thamani ya mali yako.
Twende kazi.
1. The Psychology of “Bongo Real Estate”: Kwanini Tunaogopa?
Tanzania, kama nchi nyingi za Kiafrika, bado ina Hangover ya kijamaa na mfumo dume wa kifamilia (Extended Family Pressure).
Nyumba siyo tu Asset ya kifedha; ni Status Symbol. Ukionekana unauza nyumba uliyojenga kwa jasho miaka ya 90, jamii haisemi “Ooh, anafanya Portfolio Rebalancing.” Hapana. Jamii inasema, “Mzee chuma ulete kimeisha. Ameishiwa.”
Hii “Fear of being seen as broke” inawafanya wauzaji wengi kukimbilia mafichoni. Wanataka kuuza kwa Whisper Marketing.
Tatizo la Ndugu (The “Black Tax” Factor): Hii ndiyo Real Reason namba moja. Mzee K anajua akipata hiyo 850M, na habari zikavuja kwenye Group la WhatsApp la ukoo, atapata maombi ya:
- Ada za watoto wa shangazi.
- Michango ya harusi nne.
- Matibabu ya mjomba.
- Mtaji wa biashara wa shemeji.
Mwisho wa siku, ile Capital aliyotaka kuifanyia mambo yake, inageuka kuwa National Budget ya ukoo. Hivyo, anaona bora auze kimya kimya hata kwa bei ndogo, ili abaki na amani.
Lakini je, unajua gharama halisi ya hiyo “Amani”?
2. The “Whisper Discount”: Hesabu Zinazoumiza (The Math)
Hapa ndipo nataka ufungue macho. Kwenye Real Estate, kuna kanuni moja haibadiliki:
Competition = Value. (Ushindani huleta Thamani).
Ili upate bei ya juu kabisa (Top Dollar) kwa nyumba yako, unahitaji wanunuzi wengi washindane (Bidding War). Unahitaji Buyer A ajue kuwa Buyer B anaitaka nyumba, ili Buyer A apandishe dau.
Unapochagua kuuza “Kimya Kimya” kienyeji (bila strategy), unatengeneza mazingira yafuatayo:
- Limited Exposure: Badala ya nyumba kuonekana na wanunuzi 10,000 mtandaoni, inajulikana na madalali watatu na wapambe wao.
- No Leverage: Mnunuzi anayekuja anajua yeye ndiye pekee anayejua. Hana presha. Hivyo, anaweka bei anayotaka yeye (Lowball Offer).
- Distress Signal: Hata kama hujafilisika, kitendo cha kuficha uuzaji kinatuma ujumbe kwa mnunuzi mjanja kuwa una shida au unafanya kitu cha haraka. Hii inawapa nguvu ya kukandamiza bei.
Hebu tupige hesabu halisi (Real Data Scenario):
Chukua nyumba ya Mzee K pale Mikocheni.
- Open Market Value (Kama ikiwa sokoni wazi): TZS 850 Milioni.
- Whisper Price (Mnunuzi wa siri): TZS 650 Milioni.
Kwa nini 650M? Kwa sababu mnunuzi wa siri anajua huna pa kutokea. Anajua huwezi kutangaza. Hivyo anakupa ofa ya “Take it or leave it”.
Hasara: TZS 200 Milioni.
Mzee K yuko tayari kupoteza TZS 200 Milioni (pesa ambayo ingenunua gari mpya, kiwanja kingine Kigamboni, na kusomesha wajukuu) ili tu Shangazi Nyamwiza asijue kama ameuza nyumba?
Hii inaitwa “The Fear Tax“. Ni kodi unayolipa kwa kuogopa jamii.
3. Jinsi ya Kuuza “Kimya Kimya” BILA Kupigwa (The Controlled Confidential Sale)
Kama Senior Advisor, nakubaliana na Mzee K. Siyo kila nyumba inatakiwa kupostiwa Instagram na caption ya “NYUMBA INAUZWA”. Kuna mali za mabilionea, viongozi, na watu wazito ambazo haziwezi kwenda sokoni kienyeji.
Suluhisho siyo kuuza kwa aibu. Suluhisho ni kutumia Professional Strategy.
Tunaita “Controlled Confidential Sale” au “Off-Market Listing“.
Hivi ndivyo tunavyofanya kazi na wateja wangu High Net-worth (HNWIs) jijini Dar es Salaam ili wapate bei ya soko (Market Rate) bila kelele za mtaani:
Hatua 1: The “Blind Teaser” (Kuvuta Hisia bila Kutoa Siri)
Badala ya kuweka picha ya nyumba na kusema “Nyumba inauzwa Mbezi Beach Makonde”, tunatengeneza taarifa kivuli (Blind Teaser).
Mfano wa Tangazo letu kwa Database ya Wawekezaji:
“Fursa ya Uwekezaji: Nyumba ya kifahari yenye vyumba 5, mita 400 kutoka Bahari ya Hindi, Ukanda wa Mbezi Beach. Ukubwa wa Kiwanja: 1,500 Sqm. Bei Elekezi: TZS 900M. (Strictly Confidential).”
Hapa hatujaweka picha ya geti, hatujataja jina la mtaa, wala namba ya nyumba. Ndugu yako akisoma hili, hajui ni nyumba ya nani. Lakini mnunuzi mwenye pesa (Serious Buyer), anajua hii ni spec anayotaka.
Hatua 2: Buyer Pre-Qualification (Kuchuja “Watalii”)
Kwenye uuzaji wa siri, hatutaki “window shoppers”. Hatutaki dalali anayeleta mteja wa kuja “kushangaa garden”.
Kabla ya kumpa mtu picha au kumleta nyumbani, tunafanya Vetting:
- Proof of Funds: Je, una uwezo wa kununua hii nyumba? Tuonyeshe barua ya benki au statement (iliyofutwa namba za siri).
- Identity Verification: Wewe ni nani na unafanya nini?
Hapa tunachuja matapeli na ndugu wanaopeleleza.
Hatua 3: The NDA (Mkataba wa Usiri)
Hii ndiyo silaha ya kisheria. Mnunuzi akishavuka hatua ya kwanza, tunamsainisha Non-Disclosure Agreement (NDA). Mkataba huu unasema wazi: “Ukivujisha taarifa kuwa mali hii inauzwa, au ukienda kumwambia mtu mwingine, utachukuliwa hatua kali za kisheria.”
Hii inawafunga mdomo madalali na wanunuzi. Inahakikisha Leakage ya taarifa ni sifuri.
Hatua 4: Private Viewing (Ukaguzi wa Kimya)
Mteja analetwa siku ambayo hakuna harakati nyingi. Anakuja na gari la kawaida (siyo la serikali au lenye maandishi ya kampuni). Ukaguzi unafanyika haraka na kwa weledi.
Matokeo yake? Mzee K anapata wanunuzi watatu au wanne walio “Serious” na wenye pesa mkononi. Wanashindana wao kwa wao. Mzee K anauza nyumba kwa TZS 820M (karibu kabisa na 850M), badala ya ile 650M ya “Whisper Price”.
Ameokoa heshima yake, na ameokoa TZS 170 Milioni zake.
4. Usikubali “Jamii” Iendeshe Portfolio Yako
Ndugu msomaji, nimeandika haya kwa uchungu kwa sababu naona kila siku. Naona wajane wanadhulumiwa mali kwa kuogopa kuuza wazi. Naona wastaafu wakipoteza mali zao kwa bei ya kutupwa kwa sababu ya kuogopa “maneno ya watu”.
Ukweli Mchungu (The Brutal Truth): Siku ukilala njaa, hao ndugu na majirani wanaoogopesha hawatakuja kukulipia bili zako. Siku ukishindwa kutibiwa, “Status” yako haitakulipia hospitali ya Aga Khan.
Kuuza Milki kama nyumba (Real Estate) ni mchezo wa namba, siyo hisia.
Kama unataka kuuza mali, una machaguo mawili tu:
- Uza Wazi (Open Market): Pata ushindani mkubwa, pata bei kubwa, vumilia maneno.
- Uza Kimya Kitaalamu (Controlled Sale): Tumia wataalamu, weka NDA, chuja wanunuzi, pata bei nzuri bila kelele.
Lakini usijiroge ukachagua Njia ya Tatu – ile ya kumwambia Dalali wa mtaani “tafuta mteja kimya kimya“. Hiyo ni njia ya kwenda kuchinjwa.
Hitimisho
Mzee K alipoelewa hili, tulibadilisha mbinu. Tuliingia kwenye Private Networks zangu. Ndani ya wiki 3, tulipata CEO wa kampuni moja kubwa ya Mafuta ambaye alikuwa anatafuta nyumba eneo hilo. Biashara ikaisha. Pesa ikaingia benki. Ndugu hawajui, majirani hawajui.
Mzee K sasa hivi anasimamia ujenzi wa lodge yake kijijini akiwa na tabasamu, huku mfukoni kukiwa na pesa kamili, siyo pesa iliyokatwa “Discount ya Aibu”.
Funzo: Don’t let social pressure dictate your financial destiny. Visibility is Leverage. Lakini kama lazima ufiche, ficha kwa Strategy, siyo kwa Ujinga.
Nimemaliza.